KUHUSU MWANDISHI

KUHUSU MWANDISHI

Mr. Felician Clement Meza ni mwanasayansi wa taasisi ya afya Ifakara, Wellcome Trust Fellow 2017-2020, na mwanafunzi wa udhamiri katika vyuo vya Salford na Keele vya nchini Uingereza. Ni muhitimu wa shahada ya kwanza ya sayansi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam 2013 katika masuala ya zololojia. Kazi yake kubwa kama mwanasayansi ni kufanya tafiti mbalimbali juu ya magonjwa ya binadamu ikiwemo malaria na magonjwa yasiyopewa kipaumbelea (NTDs), ili kusaidia kuzuia kuenea kwa magonjwa hayo.

Nje na kazi zake za kisayansi, ni mwanzilishi wa mtandao wa Unaweza wenye nia na malengo ya kuwahamasisha watu kubadili namna ya kufikiri na kuchukua hatua katika maisha yao. Ni mwandishi wa vitabu, makala,na machapisho mbalimbali, pia ni mchambuzi wa vitabu na machapisho ya kisayansi. Kazi zake za kisayansi na uandishi zimekuwa msaada sana kwa watu wengi hasa vijana wa kitanzania wenye kiu ya kuhamasika na kuchukua hatua ili waweze kufanikiwa katika ndoto zao.

Felician anaamini kuwa kati ya maadui watatu wa mwanadamu aliowataja Mwalimu Julius Nyerere, yaani Ujinga, Maraadhi na Umasikini. Ni adui mmoja tu ndiye anayeweza kuwa leta wenzake, ambaye ni ujinga. Ukiwa na ujinga, lazima utakuwa na maraadhi tu, na ukiwa na maraadhi ni lazima utakuwa na umasikini. Hivyo kupitia kazi zake za kisayansi, ataisaidia jamii kupambana na adui moja wapo, yaani maaradhi. Na pia kupitia kazi zake za uandishi wa makala na vitabu, ili kupambana na ujinga, Felician anaamini kuwa kila mtu anaouwezo wa kuwa anachotaka. Lakini kukosekana kwa elimu na hamasa juu ya kufanyia kazi ndoto zao kila siku, ndiyo changamoto kwa watu wengi.

Karibu sana katika mtandao wa Unaweza, tuendelee kujifunza, kuelimishana na kuchukua hatua juu ya maraadhi ujinga na umasikini, ili tuweze kuwashinda maadui hawa.  Kumbuka, Unaweza kuwa unachotaka.