Mambo matano usiyoyajua kuhusu hofu yako
Mpendwa rafiki yangu, Katika mambo ambayo yamepotoshwa sana, hofu ni moja ya mambo hayo. Siyo kupotoshwa tu, bali hata kutafasiriwa vibaya. Ukweli ni kuwa hakuna hata mtu mmoja asiyekuwa na hofu. Si wasanii wakubwa, waimbaji wakubwa, wanariadha, wafanyabiashara, matajiri au hoehae, mlala hai au mlala hoi, wote wana hofu. Lakini pia, tusingekuwa na maisha kama kusingekuwa na hofu. Hakuna kitu unachopaswa kukiogopa na kukihofia bali unapaswa kukielewa. Hivyo kama unataka kuitawala hofu yako, ndiyo kuitawala! kwan hutakiwi kushindana nayo bali…