Maeneo manne ya kuweka malengo ili upige hatua mwaka 2024

Maeneo manne ya kuweka malengo ili upige hatua mwaka 2024

Kwako rafiki mpendwa,

Heri ya mwaka mpya 2024. Tayari siku ya kwanza ya mwaka 2023 imeshakatika, je kuna kitu chochote cha tofauti ulichofanya jana kuliko ulivyofanya juzi yaani mwaka 2023?

Ni muhimu kukumbuka kuwa kinachobadilika huwa ni namba tu, kama hutabadili fikra na akili zako. Mwaka mpya kwako utakuwa ni jina tu. Sasa ushauri wangu kwa mwaka huu mpya ni kuwa na malengo makubwa, kuliko uliyokuwa umeweka mwaka jana.

Unapoweka malengo yako mapya, hakikisha unaweka malengo kwenye maeneo haya manne na kisha weka mpango au mfumo wa kuyatimiza kila siku.

Eneo la kwanza: maendeleo binafsi; hapa unahakikisha kuwa unakua kila siku. Hudhuria semina, soma vitabu kwenye eneo lako unayofanyia kazi.

Na tafuta kocha wa kukusimamia na kukuonesha njia. Hutakiwi kuwa na muda wa ukomo. Unatakiwa ukue kila siku. Kama haukui maana yake unadumaa yaani unarudi nyuma.

Eneo la pili: fedha na uchumi. Eneo hili ndilo linaweza kukusaidia kununua uhuru wako mwingine. Uhuru juu ya afya yako, muda wako, maendeleo yako binafsi na mahusiano yako, ya kimapenzi, kikazi au hata kifamilia.

Hakikisha unapoweka malengo kwa mwaka mpya, weka na mikakati ya kufanikisha malengo yako kiuchumi na kifedha.

Weka akiba, ambayo baadaye utaiwekeza ili pesa yako hiyo iwe inakuingizia kipato hata kama umelala. Na huu ndiyo uhuru wa kifedha.

Hakikisha unabana matumizi hata kama kipato chako kinaongezeka. Jue kila pesa yako inaenda wapi.

Eneo la tatu: Kiafya. Hili ni eneo ambalo ni muhimu sana kulikumbuka unapoweka malengo ya mwaka huu.

Je afya yako ya akili unamalengo gani nayo? Akili yako unailisha nini? Vitabu gani unasoma? Unapata muda wa kupumzika? Haya ni mambo muhimu kuyaweka kwenye malengo ya kuboresha afya yako ya akili.

Lakini pia afya ya kiroho unailisha nini roho yako? Unafanya tahajudi na tafakuri? Unafunga na kuomba? Ni muhimu kuwa malengo juu ya roho yako.

Bila kusahau afya ya kimwili, mwili unataka chakula kizuri, kufanya mazoezi na kupumzika. Haya lazima uzingatie unapoweka malengo yako ya mwaka huu, namna utakavyo boresha afya yako ya mwili.

Eneo la nne: Mahusiano yako. Weka malengo katika eneo hili, usilisahau. Watu wengi eneo hili huwa wanalisahau na kuliona halina umuhimu, wanakazana na kuboresha maeneo ya kifedha, kiafya na kibinafsi.

Matokeo yake inakuja kuwaghalimu sana. Mafanikio waliyoyapata kwenye maeneo mengine yanakuwa ni bure.

Wewe weka malengo kwenye mwaka huu kuboresha mahusiano yako na wewe, Mungu na mwenza wako au wale unaohusiana nao.

Rafiki, unapoweka malengo mwaka huu mpya usiyasahau maeneo haya. Lazima uwe na uzania sawa.

Usiegemee sana kwenye baadhi ya maeneo na kuacha mengine. Kwa kufanya hivyo unakaribisha matatizo ambayo baadaye utatumia mafanikio uliyoyapata kutatua matatizo hayo.

Pia ili uweze kutimiza malengo yako ya mwaka mpya na kutimiza ndoto zako, anza mwaka wako kwa kusoma kitabu cha UNAWEZA KUWA UNAYEMTAKA chenye kanuni mbali mbali za kuwa unayemtaka na kupata chochote unachotaka.

Kitabu hiki kimesheheni kanuni muhimu za jinsi ya kuweka malengo mahusi, na namna kufanya ili kuyatimiza malengo hayo.

Kupata nakala yako lipa leo elfu kumi (10000/-, elfu kumi gharama ya kitabu) piga namba 0655046577/0789383577 sasa kupata nakala yako.

Ukawe na siku njema rafiki, unapoendelea kuweka na kutimiza malengo ya mwaka mpya 2024. Ili kuendelea kupata makala hizi na huduma zetu kwenye emaili yako jiandikishe hapa chini. Pia jiunge na kundi letu la WhatsApp ilikuendelea kujifunza zaidi https://chat.whatsapp.com/LwoojycUxgpE11qCQLcosa

Felician C. Meza

Mwandishi wa vitabu

Kocha wa mafanikio na mahusiano

Mwanasayansi

© Felician Meza 2024

Meza.fc@unaweza.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *