Kwani unao au kuolewa?
Karibu rafiki kwenye tafakari yetu ya leo kutafakari kwa nini unaoa au kuolewa?. Kama ulipitwa na makala juu ya namna ya kufanya ili mwenzi wako aweze kubadilika basi isome hapa. Siku chache zilizopita nilitembelewa na rafiki yangu kutoka nchini Uswisi. Tulipata wasaa wa kuzungumza na kujadiliana mambo mbalimbali ya utofauti wa kimaisha baina yetu na wao. Moja ya swali ambalo nilimuuliza ni kwa nini watu wengi kwenye nchi yao hawako tayaari kuoa au kuolewa? Na hata kama wakioa au kuolewa…