Browsed by
Month: November 2021

Katika kutafuta mafanikio usisahau vitu hivi vitatu

Katika kutafuta mafanikio usisahau vitu hivi vitatu

Kila mtu anataka kufanikiwa kwenye maisha yake. Hata yule asiyekuwa na mipango, naye anatamani na kutaka mafanikio. Unaweza ukayatafuta na kuyapata mafaniko kweli, lakini mafanikio yako yatakuwa ni bure kabisa kama yatakosa vitu hivi vitatu. 1. Familia (au mahusiano ). Ni ukweli usiopingika kuwa unaweza ukayapata mafanikio, lakini hayatakuwa na maana kwako kama mahusiano yako na familia, marafiki na wale uwapendao, jamii na Mungu hayatawagusa kwa namna moja ama nyingine. Mafanikio ya kweli ni pamoja na kusaidia familia, marafiki na…

Read More Read More

Hivi ndivyo unaweza kuachana na umateka wa jamii

Hivi ndivyo unaweza kuachana na umateka wa jamii

Nafaahamu umuhimu wa sisi binadamu kuwa kwenye jamii, kwani ni viumbe wa kijamii. Tatizo linakuja pale jamii tunayoishi au kutokea inapokuwa kikwazo cha sisi kupiga hatua na kuwa na maisha tunayotaka kuishi. Jamii tunayoishi imeweka viwango vyake ambayo kila mwanajamii anapimwa na viwango hivyo. Kwenda kinyume (yaani zaidi ya viwango hivyo au chini ya viwango hivyo) huonekana ni usaliti kwenye jamii husika. Jamii inategemea wewe uwe na maisha ya aina fulani, kipato fulani, elimu fulani na hata kazi au biashara…

Read More Read More

Unachokitafuta unacho, lakini kimepungua…..

Unachokitafuta unacho, lakini kimepungua…..

Mara nyingi sisi wanadamu ni viumbe wa ajabu. Huwa tunahangaika kutafuta kile ambacho tunacho, na kuacha kutafuta kile ambacho hatuna. Iko hivi, kama kila siku wewe ni wakutafuta na hupati, fahamu ya kwamba hicho kitu tayari unacho ndiyo maana hukipati. Ukiwa unatafuta kitu ambacho unacho, hutaweza kukipata. Siku moja mama alinituma sindano ya kushonea nguo nimchukulie ndani. Niliingia ndani ya nyumba kweli, na kuichukua ile sindano, lakini kabla sijatoka nje likanijia wazo la kunywa maji kabisa nikiwa ndani. Ili niweze…

Read More Read More

Huyu ndiye rafiki wa kweli

Huyu ndiye rafiki wa kweli

Kama kuna rafiki ambaye hawezi kukusahau, kukutupa na kukunyanyasa basi ni kazi. Kazi ni rafiki wa kweli kwa kila mtu atakayefanya naye urafiki. Kazi ni shughuli yeyote unayoifanya iwe inakuingizia kipato ama la. Uwe unalipwa ama haulipwi, ukifanya urafiki na kazi, matokeo yataonekana tu, na asili itakulipa kwa sababu umeweka kazi. Hakikisha una kazi, shughuli au biashara inayokuingizia kipato, hata kama siyo kikubwa au hakuna kabisa, bado unautofauti na yule ambaye hafanyi kazi. Ipo siku kazi itakulipa, hata kama siyo…

Read More Read More

Fanya haya ili upate unachokitaka

Fanya haya ili upate unachokitaka

Watu wengi wanaahirisha kufanya kitu juu ya ndoto zao, mpaka wanafikia umri wa utu uzima wakiwa hawajafanya chochote juu ya ndoto zao. Mwisho wake sasa wanaanza kuwashurutisha watoto wao kutimiza ndoto zao. Katika mazingira ya kiafrika  mara nyingi nimekutana na kesi nyingi tu juu ya wazazi na watoto wao. Wazazi wanalazimisha mtoto wao asome masomo flani, lasivyo hatamlipia ada. Watoto wa namna hiyo mara nyingi wana kuwa wahanga wa ajira au hata kazi ambazo hawakuzaliwa kuzifanya. Na kama watoto hao…

Read More Read More

Usipojitambua, hakuna atakaye kutambua

Usipojitambua, hakuna atakaye kutambua

Kuna msemo maarufu wa Dr. Eli VD Waminian kuwa usipojitambua, utajitahidi kujitambulisha. Kujitambua ni kujigundua wewe umebeba nini, unathamani gani na kisha kuendelea kuijifunza kila siku ili kukiendeleza na kukitoa ulichobeba kwaajili ya wengine. Kama hujatambua thamani uliyonayo wewe kwaajili yao, na wao pia hawatatambua thamani yako, hivyo utakuwa unajitahidi kujitambulisha, lakini haitakusaidia. Kujitambua ni kugundua na kupalilia vipaji vyako, vipawa vyako na ujuzi wako, ili vig’aae kwaajili ya watu wengine, kwani wanavihitaji zaidi wenyewe. Sijawahi kuona muembe umebeba matunda…

Read More Read More

Unachokihitaji unakijua, lakini hauko tayari kuchukua hatua

Unachokihitaji unakijua, lakini hauko tayari kuchukua hatua

Ni ukweli usiopingika kwamba, kila mtu anajua anachokihitaji na kukitaka katika maisha yake, lakini changamoto ni kuwa hakuna aliyetayari kuchukua hatua. Unajua kabisa uanatakiwa ufanye nini ili ufanikiwe, lakini linapokuja suala la kuchukua hatua, hauchukui. Unajua kabisa unataka mafanikio na namna ya kuyafikia mafanikio lakini hauchukui hatua. Hebu fikiria unataka kununua bidhaa dukani, unajua kabisa nini unatakiwa kufanya. Kwanza utatakiwa kwenda dukani, hapo utatumia muda wako. Pili ukifika dukani utatatakiwa kulipa gharama ya hiyo bidhaa au huduma unayoitaka, na hapo…

Read More Read More

Wewe ni dhahabu

Wewe ni dhahabu

Ndiyo, umesoma vyema. Wewe ni dhahabu, wewe ni wa thamani. Swali unalopaswa kujiuliza ni je umeshajigundua kuwa wewe ni dhahabu? na hapa ndipo watu wengi wanapaokwama, kwani hawajijui kama wao ni dhahabu. Wao ni wa thamani. Mwili wako huo, umeficha dhahabu ndani yake, ambaye ndiyo wewe. Jukumu kubwa katika maisha yako ni kujigundua kuwa wewe ni dhahabu, wewe ni wa thamani kubwa. Kadili unavyojingundua, ndivyo ambavyo unazidi kuiongeza thamani yako. Unazidi kung’ara zaidi.  Kuna hadithi ya kweli, japo ni ya…

Read More Read More

Hiki ndicho tunakikosa kwenye elimu yetu, na namna ya kukipata

Hiki ndicho tunakikosa kwenye elimu yetu, na namna ya kukipata

Mtu yeyote asiyejiamini mwenyewe, hawezi kujitoa kafara na kulipa gharama anayotakiwa kulipa ili aweze kufanikiwa. Kama wewe hujiami, huwezi kumuamini mwezako, wala taifa lako. Hii ni kutokana na wewe ndani yako kutokuwa sawa. Mara nyingi kushindwa kutokana na sababu zilizo nje yako ni asilimia 10 tu, huku 90 zikitokana na wewe kushindwa ndani yako. Na hii ni mbaya zaidi kwani mtu asipojiamini kwamba ni wa thamani na maisha yake ni ya muhimu, atafanya ujinga mwingi kwenye maisha yake na asijue…

Read More Read More

Hata ujinga unaweza kukufikisha kwenye mafanikio, lakini hauwezi kukufanya udumu katika mafanikio hayo

Hata ujinga unaweza kukufikisha kwenye mafanikio, lakini hauwezi kukufanya udumu katika mafanikio hayo

Rafiki, bila shaka ulishawahi kuona au wewe mwenyewe kushuhudia watu wakitumia njia za mkato kuyatafuta mafanikio. Ukweli ni kuwa, hata njia za mkato zinaweza kukufikisha kwenye mafanikio lakini haziwezi kukufanya udumu kwenye hayo mafanikio. Watu hufikiri kuwa njia za mkato kwenye mafanikio huwa zinafanya kazi, lakini ukweli ni kuwa hazifanyi kazi kabisa. Unaweza ukaona unapiga hatua leo kwa sababu ya njia za mkato yaani ujanja ujanja, uongo, uzushi na ulaghai, lakini jua ya kuwa anguko lako laja. Njia za mkato…

Read More Read More