Mambo mawili ya kuzingatia ili kumpenda mwenza wako
Rafiki, kama ilivyo umuhimu wa maarifa kwenye mafanikio yoyote yale, ndivyo ilivyo pia kwenye mahusiano ya ndoa. Hivyo kukosa maarifa juu ya mwenza wako na ndoa kwa ujumla ni chanzo cha mahusiano kufa. Ujinga huwa ni hatari sana kwenye mahusiano. Migogoro na mivutano mingi kwenye mahusiano ya ndoa ni kwa sababu wengi huwa hawajuani wala kufahamiana. Huwa wanashindwa kuelewe kwamba mwanamke na mwanamume huwa wanafikiri na kuwaza tofauti, na pia huwa wanayaona na kuyatafsiri mazingira yanayoeazunguka kwa mitazamo tofauti.! Hali…