Browsed by
Month: July 2022

Je, umeshapata kitabu cha ITAWALE HOFU YAKO?

Je, umeshapata kitabu cha ITAWALE HOFU YAKO?

Rafiki, kwa muda sasa nimekuwa nakueleza kuhusu kitabu kipya nilichotoa kinachoitwa ITAWALE HOFU YAKO. Kitabu hiki nilipenda kila rafiki yangu akipate na akisome, maana nimeweka maarifa mengi na sahihi kwenye kuitawala HOFU YAKO. Hivyo niliamua kukitoa kama zawadi kwa kila rafiki yangu kwa bei ya OFA ili kukipata kitabu. ZAWADI HII INAISHA LEOHivyo nipende kutumia nafasi hii kukujulisha kama bado hujakipata kitabu hiki, chukua hatua sasa hivi ili zawadi hii isikupite. Rafiki, Waswahili wanamsemo wao maarufu usemao “Uoga wako ndiyo…

Read More Read More

Itawale hofu yako hivi

Itawale hofu yako hivi

Rafiki, haijalishi wewe ni mjanja kiasi gani, wewe ni mkubwa kiasi gani au una maono makubwa kiasi gani. Kila kitu huharibika pale unapokitazama kwa miwani na lenzi ya hofu. Hofu hupoozesha mwili wote. Hofu huuweka mwili kwenye hali ya kujiokoa, yaani survival mode. Ukitawaliwa na hofu, maana yake unakuwa kwenye hali ya kujiokoa kutoka kwenye hatari, baada ya mwili kutambua na kuona tishio la hatari au viashiri vya hatari kabla hatari hiyo haijakupata. Hofu ni wito wa kujiokoa. Hivyo, linapokuja…

Read More Read More

Je umekuwa ukitawaliwa na hofu?

Je umekuwa ukitawaliwa na hofu?

Rafiki, hofu ni hisia ya msingi kabisa kwa mwanadamu. Lakini, katika hisia zote, hisia hii ya hofu licha ya umuhimu wake kwenye maisha yetu hasa kwenye kutusaidia kujiokoa kutoka kwenye tishio la hatari au viashiria vya hatari, ndiyo hisia inayoongoza kwa kuua ndoto, maono, vipaji na makusudi ya watu wengi kwenye maisha yao. Hebu pata picha, kuna biashara ulitakiwa uianzishe miaka kadha iliyopita lakini mpaka sasa hujaianzisha kwa sababu ya hofu, ya kushindwa, kutengwa na kukataliwa. Kuna nyimbo na vitabu…

Read More Read More

Acha kutumia chote unachopata badala yake fanya hivi

Acha kutumia chote unachopata badala yake fanya hivi

Rafiki, kama unachokipata, unakitumia chote unafanya makosa. Mafanikio yoyote yale hasa ya kifedha, hayapimwi kwa kiwango unachopata au kupokea, bali kinapimwa kwa kiwango kile unachoweka kama akiba na kukiwekeza. Kile kinachobaki mikononi mwako baada ya matumizi yako. Kila pesa inayopita mikononi mwako, hakikisha huitumii yote. Hakikisha unaweka akiba sehemu ya pesa hiyo, hata kama ni kiwango kidogo sana. Ni kawaida kujiambia kuwa nikiwa napata kiwango kikubwa cha pesa ndiyo nitaweza kuweka akiba na kuwekeza. Lakini mambo huwa hayako hivyo, kwani…

Read More Read More

Unahasira? Itawale hasira yako kwa kufanya hivi

Unahasira? Itawale hasira yako kwa kufanya hivi

Rafiki, watu wengi hufikiri kuwa kile wanachofanyiwa au kutendewa ndiyo chanzo cha hasira yao. Lakini ukweli ni kwamba kile unachofanyiwa au kutendewa na kupelekea wewe kushikwa na hasira huwa ni kichocheo tu cha hasira yako. Siyo chanzo au sababu ya wewe kuwa na hasira. Kinachofanya watu wengi kutawaliwa na hasira siyo kile walichotendewa, bali ni kile wanachofikiria, kutafakari na kukitolea hitimisho kwenye fikra zao. Pale unapopatwa na hasira, unapaswa kujiuliza nini chanzo au kisababishi cha hasira yako? Chanzo hicho kiko…

Read More Read More

Usiingie kwenye ndoa kwa kujaribu bali fanya hivi

Usiingie kwenye ndoa kwa kujaribu bali fanya hivi

Rafiki, miaka ya nyuma kidogo nilinunua kamera mtandaoni, si unajua tena mambo ya kununua vitu mtandaoni ndiyo yalikuwa yanaingia huku kwetu na ilikuwa ni kitu kigeni sana. Basi bwana nilikuwa na furaha isiyo kifani baada ya kupokea mzigo wangu huo ukiwa umefungwa vizuri ndani ya boksi. Sasa ulifika muda wa kufungua boksi na kuangalia kilichomo ndani. Kweli kamera ilikuwa ni ile ile niliyoiona mtandaoni, lakini kuna kitu muhimu kwenye boksi hakikuwemo! Unajua ni nini hakikuwemo kwenye boksi? Hakukuwa na kitabu…

Read More Read More

Mahusiano yako ya ndoa umeyajenga kwenye msingi gani?

Mahusiano yako ya ndoa umeyajenga kwenye msingi gani?

Rafiki, mahusiano ya ndoa yanayodumu kwa muda mrefu na kuwa na furaha na amani yanatokana na kujengwa kwenye msingi imara. Msingi imara ni ule usioteteleka, usiooza wala kumomonyoka. Msingi ambao unajengwa kwenye vitu vinavyodumu badala ya kupita. Usijenge mahusiano yako ya ndoa kwa kutegemea uzuri wa mwili, kwani uzuri huwa haudumu. Nywele hubadilika, rangi ya ngozi hufubaa na kusinyaa. Kuona kunapungua, kusikia nako kunapungua. Meno hung’ooka na mwili hupungua au kuongezeka. Kama ndoa na mahusiano yako umeyajenga kweny uzuri na…

Read More Read More

Maadalizi ni muhimu kwenye mafanikio, lakini usisahau hiki

Maadalizi ni muhimu kwenye mafanikio, lakini usisahau hiki

Rafiki, ni kweli unahitaji maadalizi kwenye kila kitu unachokifanya, lakini unahitaji kuchukua hatua pia. Mafanikio ya nahitaji mtu uchukue hatua, hata kama ni ndogo kiasi gani wewe fanya hivyo hivyo kwa udogo wake. Maandalizi mazuri ni yale unayoyafanya, huku unachukua hatua. Unafanyia kazi yale unayojiandaa nayo. Kama ni kusoma vitabu, unapaswa usome na kuanza kufanyia kazi mara moja yale unayojifunza. Kama ni kufanya biashara, unapaswa kujiandaa, huku ukifanya biashara. Usisubiri mpaka ufikie hatua ya juu, au mpaka uwe na kila…

Read More Read More

Hii ni sababu isiyofaa kwa wewe kuingia kwenye mahusiano ya ndoa

Hii ni sababu isiyofaa kwa wewe kuingia kwenye mahusiano ya ndoa

Rafiki, huwa kuna sababu za msingi, nzuri na bora za kuingia na kuanzisha mahusiano ya ndoa yatakayo dumu. Lakini pia huwa kuna sababu za hovyo, mbaya ambazo mtu hutakiwi kuingia kwenye mahusiano ya ndoa kwa sababu hizo. Ndoa nyingi siku hizi zinashindwa kufanikiwa na kudumu kwa sababu ya wanandoa wenyewe kutokujua kusudi hasa la ndoa ni nini? Na ni kanuni zipi zinafanya ndoa yenyefuraha, amani na upendo iweze kudumu? Kamwe hutakiwi kabisa kuingia kwenye mahusiano ya ndoa bila kuwaza kwa…

Read More Read More

Tatizo lako si kupata bali ni hili

Tatizo lako si kupata bali ni hili

Rafiki, tatizo la watu wengi siyo kupata bali kumiliki. Kama ni kupata pesa, watu wanapata sana, lakini kwenye kuzimiliki na kuzitunza ni shughuli. Kama ni biashara watu wanafanya sana, lakini tatizo ni kuzimiliki na kuzitunza ndiyo kazi kubwa. Kama ni ndoa watu wanafunga kila siku lakini tatizo ni kuzimiliki na kuzitunza ndoa zao. Kama ni kazi watu wanapata sana, lakini tatizo ni kuzimiliki na kuzitunza kazi zao hizo. Mifano ni mingi sana, lakini itoshe tu kukwaambia kuwa tatizo lako siyo…

Read More Read More