Mambo muhimu ya kujifunza kutoka kwa Mandoga
Mpendwa rafiki, Sina uhakika kama unamfahamu au ulishawahi kumsikia lakini kuna vitu vyingi muhimu vya kujifunza kutoka kwake.Huyu si mwingine bali ni bondia aliyejizolea maarufu sana siku za hivi karibuni nchini Tanzania. Alianza kama utani wakambeza, wakamcheka na wengine kumdharau na kumdhihaki pengine kwa sababu ya umri wake kuwa mkubwa, au kutokuwa na hisitoria yoyote kwenye mchezo wa ngumi si mwingine bali ni Karim Mandonga. Kwasasa Mandonga anaushawishi mkubwa kwenye ndondi pengine kuliko bondia yeyote hapa Tanzania. Si Mwakinyo, Dulla…