Maeneo manne ya kuweka malengo ili upige hatua mwaka 2024
Kwako rafiki mpendwa, Heri ya mwaka mpya 2024. Tayari siku ya kwanza ya mwaka 2023 imeshakatika, je kuna kitu chochote cha tofauti ulichofanya jana kuliko ulivyofanya juzi yaani mwaka 2023? Ni muhimu kukumbuka kuwa kinachobadilika huwa ni namba tu, kama hutabadili fikra na akili zako. Mwaka mpya kwako utakuwa ni jina tu. Sasa ushauri wangu kwa mwaka huu mpya ni kuwa na malengo makubwa, kuliko uliyokuwa umeweka mwaka jana. Unapoweka malengo yako mapya, hakikisha unaweka malengo kwenye maeneo haya manne…