Hiki ndicho kikwazo kimoja cha wewe kutokufanikiwa au kufanikiwa
Rafiki yangu karibu sana kwenye tafakari yetu ya leo, tutafakari ujumbe huu kwa kina “Hiki ndicho kikwazo kimoja cha wewe kutokufanikiwa au kufanikiwa” Siku moja nikiwa nimejipumzisha ndani kwangu majira ya jioni. Nyuma ya nyumba yangu kulikuwa na mafundi ujezi wakiwa wanaendelea na ujezi wa nyumba ya jirani yetu. Wakati wakiendeleana ujezi kulitokea ubishani, juu ya kuamini. Fundi mmoja alikuwa akiwambia mafundi wezake kuwa yeye haamini kama Mungu yupo. Wezake walijitahidi sana kumuelimisha nakumuonyesha mambo makuu ya Mungu, lakini hakuwaelewa,…