Siri ya mafanikio ni kufanya kile usichojisikia kufanya
Kwako rafiki mpendwa, Nafahamu kwamba wewe huwa unafanya kile unachokuwa unajisikia kufanya; ndiyo maana uko hapo ulipo leo. Biashara zako haziendi, kazi zako haziendi, mahusiano yako yamekwama na maisha yako siyo mazuri. Unafanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa lakini bado mambo ni magumu. Habari njema ni kwamba leo na kwenda kukushirikisha siri moja muhimu ambayo itabadili kabisa biashara yako, kazi yako, mahusiano yako na maisha yako kwa ujumla. Ni siri ambayo hakuna serikali, ndugu, jamaa na rafiki aliyetayari kukwambia….