Unataka kuwa nani? unataka nini kwenye maisha?
Rafiki yangu, mara nyingi ukiwauliza maswali watoto wadogo kuwa wanataka kuwa nani au kufanya nini wakiwa watu wazima watakujibu moja kwa moja bila hada kusita sita. Lakini ukiwauliza watu wazima, utashangaa ni kwa namna gani wanavyosita sita. Hii inatokana na kwamba, watu wazima tayari walisha anza kuona na kuamini kuwa hawata weza kufanikiwa kwa kile wanacho taka au wanachofikiria kuwa. Hivyo, uoga wa kushindwa na hofu ya kukabiliana na changamoto zinazo ambatana na kile wanachokitaka huwa zinawafanya washindwe kuwa bayana…